SERIKALI imetakiwa kusitisha zoezi la kupandisha nauli za mabasi
na daladala zinazotarajiwa kuanza kutumika Aprili 12, mwaka huu.
Akizungumza na chanzo chetu Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa
Morogoro, Susan Kiwanga, alisema serikali inapaswa kuwashirikisha
wanachi juu ya mipango yake ili kuepusha mabishano.
Akitoa mfano, alisema kuwa kupanda kwa gharama hiyo kutawafanya
wanachi hususan asilimia 80 waliopo vijijini kuendelea kuwa fukara na
wengine kupoteza maisha kwa kushindwa kumudu gharama za maisha
zinazopandishwa na mfumo mzima wa usafirishaji.
“Serikali lazima iandae mazingira mazuri kwa watoa huduma kama kuondoa
kodi na ushuru kwenye vipuli na mafuta, na kuboresha barabara, mfano
barabara za vijijini,” alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jahazi Asilia Mkoa wa Morogoro, Ismail
Rashidi, alisema serikali imekuwa ikijichanganya katika kupambanua hali
ya uchumi ikidai uchumi unapanda kwa asilimia saba wakati uhalisia wa
pato la Mtanzania ni asilimia tatu.
“Kupandishwa kwa gharama hii ni pigo kwa Watanzania wengi hususan wa
vijijini kwa kuwa wanategemea zaidi vyombo vya usafiri kuboresha maisha
yao kama kusafirisha mazao na kuja mijini kununua mahitaji ya kijamii,”
alisema.
"Chanzo Tanzania Daima"
|
0 comments:
Post a Comment