Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Friday, 26 April 2013

Misikiti yashambuliwa Iraq, wanne wauawa
Watu wanne wameuawa na makumi na wengine wakiwemo raia, askari polisi na wanajeshi wa Iraq kujeruhiwa hii leo Sambamba na kuendelea kwa mashambulizi ya kigaidi mjini Baghdad na maeneo mengine ya nchi hiyo.
Vyanzo vya usalama na hospitali nchini Iraq vimetangaza kuwa, mashambulizi hayo katika misikiti kadhaa mjini Baghdad yameua watu 4 na kujeruhi wengine 50.
Wakati huo huo, polisi ya Iraq pia imetangaza kutokea mlipuko mwingine katika msikiti ulio katika eneo la Al-Biyaau, kusini mwa mji mkuu Baghdad. Weledi wa masuala ya kisiasa wameyataja mashambulizi hayo kuwa, yana lengo la kuzusha fitna za kimadhehebu kati ya Waislamu nchini humo.


0 comments:

Post a Comment