Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 27 April 2013

Jaji wa ICC ajiondoa kesi ya Uhuru, Rut

Kesi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Naibu wake William Ruto  katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imeendelea kuporomoka baada ya jaji mmoja kujiondoa.
Imearifiwa kuwa Aprili 8 mwezi huu Jaji Christine Van den Wyngaert raia wa Ubelgiji ameomba kujiondoa kama jaji  katika kesi ya Uhuru na Ruto. Kwa mujibu wa tovuti ya ICC, kabla ya kujiondoa Jaji Bi. Wyngaert alishambulia vikali upande wa mashtaka kutokana na usimamizi mbovu wa kesi. Amesema kuna maswali magumu iwapo kweli upande wa mashtaka ulitekeleza uchunguzi kamili dhidi ya washukiwa kabla ya kesi kuanza. Aidha amesema ofisi ya mwendesha mashtaka wa ICC haina kusingizio chochote kuhusu kushindwa kwake kuchunguza iwapo ushahidi uliowasiliwha mbele ya mahakama unaweza kuaminika au la. Mashahidi kadhaa muhimu waliokuwa wamepangwa kutoa ushahidi dhidi ya rais Kenyatta wameshajiondoa. Mwendesha Mashtaka wa ICC anadai kuwa  Uhuru, Ruto na mwandishi habari Joshua Sang walihusika katika ghasia za baada ya uchaguzi Kenya mwaka 2007. Hatahivyo wote hao wamekanusha vikali madai hayo ya ICC. 

0 comments:

Post a Comment