Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday 6 April 2013

MBUNGE MWIDAU AHAMASISHA MIRADI YA MAENDELEO TANGA

                             26,Jumaadal ula,1434Hijiriyah/ April 07,2013Miyladiyah

Mbunge Mwidau akisalimia na wanawake wa kikundi cha wajasiriamali wafugaji wa kuku wa Kata ya Pongwe kijiji cha Marizara.
     
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), kiakabidhi mpira kwa kiongozi wa timu ya Kata ya Kiomoni, Mohamed Said huku baadhi ya mashabiki wakishuhudia upokeaji wa mpira huo.

Mbunge Mwidau, akisalimia na wanawake wa Kata ya Mafuriko, ambao walifika kumlaki katika ziara yake ya Wilaya ya Tanga
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), akipata maelezo ya mradi wa kisima cha maji kutoka kwa Diwani wa Kata ya Mwera Maisha Mkaidi (CUF), wengine ni baadhi ya viongozi na wananchi wa kata hiyo.
Mbunge Mwidau, akikabidhi fedha kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipumbwi Jamali Nassoro kwa ajili ya kununua mifuko kumi ya saruji ikiwa ni sehemu ya ahadi ya mbunge katika kuunga mkono ujenzi wa shule ya Msingi Kipumbwi Pwani.
Mbunge Mwidau akikabidhi mifuko kumi ya saruji kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Msambweni Bahati Marungu kwa ajili ya ujenzi shule ya Sekondari ya Kata ya Msambweni.
 
wa yakitokea nchini yamekuwa yakipangwa na kuratibiwa na viongozi wa chama hicho kutimiza ahadi yao ya kuhakikisha nchi haitawaliki.

Mbunge Mwidau akisalimia na wanawake wa kikundi cha wajasiriamali wafugaji wa kuku wa Kata ya Pongwe kijiji cha Marizara.
Mbunge Mwidau, akisalimia na wanawake wa Kata ya Mafuriko, ambao walifika kumlaki katika ziara yake ya Wilaya ya Tanga
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), akipata maelezo ya mradi wa kisima cha maji kutoka kwa Diwani wa Kata ya Mwera Maisha Mkaidi (CUF), wengine ni baadhi ya viongozi na wananchi wa kata hiyo.
Mbunge Mwidau, akikabidhi fedha kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipumbwi Jamali Nassoro kwa ajili ya kununua mifuko kumi ya saruji ikiwa ni sehemu ya ahadi ya mbunge katika kuunga mkono ujenzi wa shule ya Msingi Kipumbwi Pwani.
Mbunge Mwidau akikabidhi mifuko kumi ya saruji kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Msambweni Bahati Marungu kwa ajili ya ujenzi shule ya Sekondari ya Kata ya Msambweni.
Mbunge wa Mwidau, akikagua madarasa ya shule ya Sekonadari ya Msambweni, kulia ni Diwani wa Kata ya Msambweni Abdulrahaman Hassan (CUF).
.....................................................................................
 
MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), awametaka wananchi wa mkoa wake kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Kauli hiyo aliitoa kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza katika ziara yake hiyo katika kata za halmashauri ya jiji la Tanga na Wilaya ya Pangani, ambapo alisema ni muhimu kwa kila mwanajamii kutambua wajibu wake.
“Suala la amaendeleo halina itikadi na sasa sio wakati wa kampeni za uchaguzi, ni jukumu letu kwa viongozi wa Mkoa wa Tanga, kuhakikisha tunashiriki katika miradi ya maendeleo kwa dhati.
“Ni wazi Mkoa wa Tanga tuna kila sababu ya kuhakikisha tunaimarisha uchumi wetu hasa baada ya miaka kadhaa viwanda vyake kufa kutokana na kutokuwepo na usimamizi mzuri.

Ikiwa kila mtu atatambua wajibu wake ni wazi tutafanikiwa kufikia lengo letu,” alisema Mwidau.
 Alisema kutokana na hali hiyo kila mara amekuwa akishiriki katika kuhamasisha maendeleo katika maeneo yote ya mkoa huo bila kujali uongozi wa kaa upo chini ya chama cha CUF au CCM.
 
 “Tanga tuna ardhi nzuri na tuna kila sababu ya kujivunia jambo  hili ingawa kukosekana kwa usimamizi madhubuti kwetu imekuwa ni kilio kikubwa kwa wananchi wetu tunaowaongoza, wabunge wote wa mkoa huu tuna wajibu wa kuliangalia hili,” alisema Mbunge Mwidau.
 
Katika ziara hiyo akiwa wilayani Pangani Mwidau, alisema kuwa amefurahishwa kuona wananchi na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mwera kuamua kuchimba kisima kikubwa zaidi ya kilichopo sasa na katika hilo amefurahishwa kuona mchango wa awali wa mashine aliyoitoa imewezesha kujengwa kwa kisima kisima kingine kikubwa cha futi 45 na kipenyo cha nchi sita.
 
"Habari hii ni hisani ya Francis Godwin bloga"

0 comments:

Post a Comment