Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 30 April 2013

Malaki wapoteza maisha kwa balaa la njaa Somalia



Zaidi ya watu laki mbili na elfu sitini wamefariki dunia nchini Somalia  nusu yao wakiwa ni watoto walio na umri wa miaka mitano kutokana na kukabiliwa na balaa la njaa katika kipindi cha mwaka 2011.
Taarifa zinasema kuwa, kutochukuliwa hatua za haraka za kupelekwa misaada ya kibinadamu kwa wakati mwafaka, kumechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa vifo hivyo. Ripoti hiyo iliyotayarishwa na taasisi ya FEWS NET imeeleza kuwa, wahanga wakubwa wa balaa hilo walikuwa wanawake na watoto.
Somalia inahesabiwa kuwa moja kati ya nchi zenye idadi kubwa ya wakimbizi duniani, hali iliyochangiwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya zaidi ya miongo miwili.

0 comments:

Post a Comment