Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 2 April 2013

Kongamano la kurekebisha mahakama laanza Somalia

                                                                    21,Jumaadal ula,1434Hijiriyah/ Murch 02,2013Miyladiyah
                                                                                
Kongamano la kitaifa lenye shabaha ya kuufanyia marekebisho mfumo wa mahakama nchini Somalia limeanza rasmi nchini humo.
Taarifa kutoka Mogadishu zinaeleza kuwa, wanasheria, wawakilishi  kutoka taasisi  na asasi za  sheria, waendesha mashtaka na wanachuoni wa kidini nchini Somalia walianza mkutano wao jana kwa shabaha ya kuufanyia marekebisho mfumo wa mahakama nchini humo.
Katika hotuba ya ufunguzi wa kongamano hilo, Rais Hassan Sheikh Mahmoud wa Somalia alisema kuwa, lengo la kongamano hilo ni kuboresha hali ya vyombo vya mahakama na kunyanyua kiwango cha ubora wa mahakimu.
Wajumbe wa kongamano hilo watajadili kwa kina suala la kuangaliwa upya hali ya vyombo vya mahakama nchini Somalia, suala la kutolewa mafunzo kwa wafanyakazi wa mahakama na mfungamano uliopo baina ya sheria za Kiislamu na sheria za taifa la Somalia.

0 comments:

Post a Comment