Mkuu wa Jeshi la utawala haramu wa Israel, ametishia kuanzisha
mashambulizi mapya dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Kwa mujibu wa ripoti
iliyotolewa leo na redio ya Israel, Benny Gantz amesema kuwa, vikosi vya
utawala wa Kizayuni vinakusudia kuanzisha operesheni kubwa ya kijeshi
dhidi ya ukanda huo, kushinda mashambulizi ya siku nane yaliyofanywa na
Israel mwishoni mwa mwaka jana. Kuhusiana na uwezekano wa kuanza kwa
Itifadha ya Tatu katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan,
Gantz amekiri kuwa, hivi sasa Israel inakabiliwa na changamoto kubwa,
tofauti kabisa na changamoto ulizowahi kukabiliana nazo utawala huo wa
Kizayuni. Ni vyema kukumbusha hapa kwamba, katika mashambulizi ya siku
nane ya Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza, yaliyoanza katikati ya mwezi
Novemba mwaka 2012, Wapalestina wasiopungua 190 waliuawa shahidi na
maelfu ya wengine kujeruhiwa.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment