Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Friday 11 January 2013

WAISLAM WATAKA HAKI ZAO KATIKA KATIBA MPYA

TAASISI ya Jumuiya ya Waislamu na Taasisi za Kiislam, zimetaka Katiba mpya itamke kuwepo na chombo cha kisheria kitakachosimamia na kuwa na mamlaka ya kusikiliza masuala ya Kiislamu.
Maoni hayo yaliwasilishwa jana jijini Dar es salaam kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na viongozi wa taasisi hizo waliowakilishwa na Sheikh Musa Kundecha.
Kundecha alifafanua kuwa wametaka Katiba mpya iwe na chombo hicho na kwamba mchakato wake ufanyike kwa umakini ili kuepusha ucheleweshaji kama ilivyokuwa katika Mahakama ya Kadhi.
Pia walipendekeza kuwa mawaziri wote wasiwe wabunge bali wachaguliwe na taasisi, asasi, vyama vya siasa na viongozi wengine.
Aidha Kundecha alisema wamependekeza Katiba mpya itoe uhuru wa elimu ya dini katika mashule yote.
Pia suala jingine ambalo walitaka litamkwe katika Katiba ni kutaka waumini wa Kiislam, siku ya Ijumaa wafanye kazi nusu siku.
Alisema kuwa siku ya Ijumaa ni siku ya ibada hivyo Waislamu wanatakiwa wapewe mapumziko.
Aidha Sheikh Kundecha alisema kuwa amependekeza kutenganishwa kwa vyeo vya ubunge na uwaziri ambapo alisema hali hiyo inasababisha kuwepo kwa upendeleo wa maendeleo katika maeneo mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment