Marekani, ikishirikiana na baadhi ya nchi za eneo ikiwemo Saudi Arabia,
Qatar na Uturuki zinajaribu kuzusha machafuko ya ndani nchini Iraq ili
kuvuruga amani na uthabiti na kuigawa nchi hiyo. Shirika la habari la
Iraq la an Nakhil limeripoti kuwa ghasia zilizotokea katika majuma
kadhaa yaliyopita kwenye baadhi ya miji ya Waislamu wa Kisuni nchini
humo kama al Anbar, Nainawa na Salahuddin zimechochewa na mirengo yenye
mfungamano na madola ya kigeni, kwani viongozi wa Marekani wanatekeleza
njama dhidi ya serikali ya Iraq inayoongozwa na Waislamu wa Kishia kwa
kuzichochea Saudi Arabia na Qatar dhidi ya serikali hiyo, na sababu ni
kwamba Washington inahisi kuendelea kubaki madarakani Waziri Mkuu wa
Iraq Nouri al Maliki kunakinzana na maslahi yake katika eneo hili la
Mashariki ya Kati.
An Nakhil limeashiria uungaji mkono wa serikali ya
Iraq kwa Rais Bashar al Assad wa Syria na kufafanua kuwa maandamano
yaliyoratibiwa, ambayo yamefanyika katika maeneo kadhaa ya Iraq chanzo
chake ni mitazamo ya serikali ya al Maliki kuhusiana na kadhia ya Syria,
na kimsingi ni kwamba kwa kuishinikiza serikali ya Baghdad na
kuichochea baadhi ya mirengo ya Iraq dhidi ya serikali hiyo, Saudia,
Qatar na Uturuki zimekuwa na nafasi kuu katika ghasia na machafuko
yanayoshuhudiwa nchini Iraq.
Wakati huohuo Salman al Musawi, mwanachama
wa mrengo wa 'Utawala wa Sheria' katika bunge la Iraq amefichua kuhusika
kwa Marekani, Saudi Arabia na Qatar katika maandamano dhidi ya serikali
yanayofanyika nchini Iraq na kusisitiza kwamba bunge la nchi hiyo
litachukua hatua kuhusiana na nchi zinazochochea ghasia na machafuko
nchini humo.
Mbali na wanasiasa, viongozi wa kidini wa Iraq pia
wanaamini kuwa ghasia za hivi karibuni nchini humo zimechochewa na
madola ya kigeni. Sheikh Mahdi Karbalai, mwakilishi wa Marjaa Mkuu wa
Waislamu wa Kishia nchini Iraq Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Sistani
amezituhumu baadhi ya nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi kuwa
zinachochea vurugu ili kuvuruga utulivu na uthabiti nchini Iraq.
Sheikh
Mahdi Karbalai, ambaye ni Khatibu wa Sala ya Ijumaa katika mji mtakatifu
wa Karbala ametahadharisha juu ya njama za nchi hizo na kuyataka
makundi ya kisiasa ya Iraq kutatua matatizo yao ya ndani kwa kuzingatia
maslahi ya taifa na kuweka kando matashi ya kikoo na kikaumu. Wakati
huohuo katika hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali ya Waziri Mkuu
Nouri al Maliki kwa lengo la kurejesha utulivu kikao cha kwanza cha
kamati ya Baraza la Mawaziri ya kufuatilia matakwa ya waandamanaji
kimefanyika nchini humo.
Itakumbukwa kuwa mnamo mwezi uliopita wa
Desemba na kufuatia kutiwa nguvuni walinzi wa Waziri wa Fedha wa Iraq
Rafi'i al Issawi kwa tuhuma za kufanya vitendo vya kigaidi, baadhi ya
makundi ya kisiasa nchini humo hususan la Faharasa ya al Iraqiyyah
linaloongozwa na Iyad Allawi na kwa uungaji mkono wa Saudi Arabia, Qatar
na Uturuki yalichochea maandamano dhidi ya serikali katika baadhi ya
miji ya Iraq ya Waislamu wa Kisun
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment