Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 12 January 2013

MATUKIO YA PICHA KATIKA KILELE CHA MAPINDUZI UWANJA WA AMANI MJINI ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikagua gwaride la Vikosi vya ulinzi katika kilele cha sherehe za kutimiza Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wakati alipomaliza
kukagua gwaride la  Vikosi vya ulinzi katika kilele cha sherehe za
kutimiza Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo
katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja



Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita na kutoa heshima mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Maraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein wakati wa maadhimisho ya miaka 49 ya mapinduzi ya Zanzibar.
 


 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, akikagua Gwaride wakati wa Sherehe za Mapinduzi, zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar



 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ameir Pandu Kificho, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza  na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar  

0 comments:

Post a Comment