Rais
Shein ameyasema hayo leo alipokuwa akilihutubia Taifa katika kilele cha
sherehe za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar kilichofanyika
Uwanja wa Amani mjini Zanzibar.
Amesema
ushirikaiano wa Serikali na wananchi umeipatia Zanzibar mafanikio
mazuri katika kuimarisha uchumi wake ambao mwenendo wake umeliwezesha
pato la Taifa kufikia Shilingi Bilioni 1,198 mwaka 2012 kutoka Bilioni
946 mwaka 2011.
Amefahamisha
kuwa mafanikio hayo yametokana na kukua kwa Sekta ya Uvuvi, Biashara na
ujenzi wa Mahoteli na Mikahawa jambo ambalo limesaidia Serikali
kupunguza mfumko wa bei kutoka asilimia 20 mwaka 2011 hadi asilimia 4.2
mwaka 2012.
Kuhusu
Kilimo Rais Shein amesema Serikali yake inaendelea kuchukua juhudi
mbali mbali za kukiendeleza kilimo ikiwemo kuimarisha Miundombinu ya
kilimo cha umwagiliaji ili kuhakikisha kuwa Hekta 8,521 za Unguja na
Pemba zinatumika kwa ajili ya kilimo hicho.
Aidha
ameongeza kuwa Serkali inaendelea na azma yake ya kulinda hadhi ya zao
la Karafuu ambapo mkakati wa kupatikana kwa Utambulisho maalum wa
Karafuu za Zanzibar (Branding) upo katika hatua nzuri.
Amewahimiza
Wakulima kupanda Mikarafuu kwa wingi na kuyatunza mashamba yao na
kuachana na tabia ya kuuza Karafuu kwa njia ya magendo.
Kuhusu
maslahi ya Wafanyakazi Dkt. Shein amesema Serikali inaendelea
kuimarisha maslahi bora kwa watumishi wote na kuimarisha mishara na
stahili nyingine za wafanyakazi kadri hali ya uchumi itakavyoruhusu ili
kuendesha vyema maisha yao.
Kuhusu
Muungano Dkt. Shein amewahakikishia wananchi wote kwamba Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika kuendeleza Muungano huo na kuwatumikia
wananchi wote.
Akitoa
salamu zake Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe hizo ambaye pia Makamo wa
Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd amesema jumla ya Miradi ya kimaendeleo
53 yenye thamani ya Shilingi 97.4 Bilion imezinduliwa katika shamra
shamra za kusherehekea miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Awali
Rais Shein alipokea Salamu za Rais na Gwaride maalum kutoka Vikosi vya
Ulinzi na Usalama pamoja Vikosi vya SMZ, Maandamano ya Wananchi na
Taasisi mbalimbali za Serikali ambapo pia Jumla ya Mizinga 21 ilipigwa
kuhanikiza sherehe hizo.
Sherehe
hizo zilihudhuriwa na Viongozi wa kitaifa akiwemo Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete,Makamo wa Rais Dkt. Gharib
Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Maalim Seif Shariff Hamad,Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd, Marais
wastaafu, Mawaziri, Mabalozi, Viongozi mbalimbali na Wananchi wa
Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment