Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday, 22 October 2012

Kushambulizi Israel meli ya misaada ni uharamia

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwamba, shambulizi lililofanywa na vikosi vya majini vya Israel dhidi ya meli ya misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wakazi wa Gaza ni sawa kabisa na uharamia na kukiuka wazi haki za binadamu. Ramin Mehmanparast amesema hayo sambamba na kulaani hatua hiyo ya vikosi vya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel ya kushambulia meli ya Estelle iliyokuwa imebebea misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wananchi wa Palestina wa Ukanda wa Gaza wanaoishi katika mzingiro wa utawala huo ghasibu. Mehmanparast amezitaka mahakama za kimataifa kufuatilia uhalifu huo na kitendo cha kutekwa nyara wanaharakati wa haki za binadamu na meli hiyo pamoja na kuchukuliwa hatua za haraka ili kuzuia dhulma wanayofanyiwa wakazi wa Gaza. Meli hiyo ya Sweden iliyokuwa imebeba misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wakazi wa Gaza ilishambuliwa na jeshi la Israel Jumamosi iliyopita na kuzuiwa kutia nanga katika pwani ya Ukanda wa Gaza na hivi sasa inashikiliwa na Israel. Mwaka 2010 katika tukio kama hilo Israel pia ilishambulia meli ya misaada ya Uturuki katika maji ya kimataifa na kuwaua wanaharakati 9 na kuwajeruhi wengine kadhaa.

0 comments:

Post a Comment