Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 4 July 2013

Jeshi la Misri lamuuzulu Mursi





Jeshi la Misri limemuuzulu Rais Muhammad Mursi wa nchi hiyo na kusimamisha katiba, hatua ambayo imechukuliwa ili kututua mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa maafisa wa ngazi za juu wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri, Mursi anashikiliwa katika jengo la Wizara ya Ulinzi pamoja na wasaidizi wake wa ngazi za juu.
Jeshi la Misri limetoa taarifa ya kusimamishwa katiba na kuteuliwa aliyekuwa mkuu wa Mahakama Kuu ya Katiba Adly Mansour kuwa kiongozi wa mpito wa Misri. Mansour anatarajiwa kuapishwa hii leo.
Wakati huo huo watu wasiopungua 14 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa nchini Misri katika machafuko yaliyotokea kati ya wanaomuunga mkono Musri na wanaopinga baada ya jeshi kumuondoa madarakani kiongozi huyo.
Katika upande mwingine kiongozi wa upinzani Mohamed al Baradei amesema, ramani ya njia iliyotangazwa na jeshi la Misri inakidhi matakwa ya wananchi ya kufanyika uchaguzi wa mapema.


0 comments:

Post a Comment