Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 4 July 2013

Adhana kwenye televisheni ya Uingereza

 Wakati unakaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa mara ya kwanza kabisa kanali ya 4 ya televisheni ya nchini Uingereza itakuwa ikirusha hewani moja kwa moja adhana ya sala ya asubuhi.
Justine Bower mkurugenzi wa masuala ya umma wa kanali ya 4 ya televisheni ya nchi hiyo amesema kuwa, kanali hiyo itakuwa ikirusha moja kwa moja adhana ya asubuhi kwa ajili ya wananchi wa Uingereza. Ameongeza kuwa, waumini wa dini ya Kiislamu wapatao milioni mbili na laki nane nchini humo wataanza mfunguo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani siku chache zijazo. Bower amesema kuwa kanali hiyo pia itakuwa ikirusha hewani adhana kupitia mtandao wa kanali hiyo.
 Alipoulizwa wamejiandaa vipi kukabiliana na ukosoaji kwa hatua hiyo, Justine Bower amesema kuwa, karibu asilimia 5 ya wananchi wa nchi hiyo wako katika pirika za kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Amesema kuwa, mwezi wa Ramadhani hufungwa na waumini wa dini ya Kiislamu kila mwaka, na nitawashangaa watu watakaostaajabishwa na uwepo wa utambulisho huo wa kidini. 

0 comments:

Post a Comment