Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 25 June 2013

‘White House’ yataja sifa za Obama kuja nchini

  Ukitaka kumfahamu mtu, tazama aina ya watu wanaomzunguka. Msemo huu unaweza kutumika kuielezea Tanzania hasa baada ya kupata fursa ya kutembelewa na marais wawili wa taifa lenye nguvu zaidi duniani.
Mara ya kwanza, Tanzania ilitembelewa na Rais wa Marekani aliyekuwapo madarakani, Bill Clinton, Agosti 28 hadi 29, 2000.
Pia, nchi ikapata tena fursa ya kutembelewa na Rais George Bush mwanzoni mwa 2008 na sasa nchi imepata fursa tena ya kutembelewa na rais mwingine wa nchi hiyo, Barack Obama, ambaye atakuwa ameambatana tena na Bush, jambo ambalo ni la kihistoria kwa bara hili.
Licha ya kuwapo hali ya kutoridhika na hali halisi ya nchi, kiuchumi, kisiasa na kijamii kutoka kwa baadhi ya Watanzania, hali inaonekana tofauti kwa Marekani ambayo mtazamo wake wa masuala ya nchi za nje unawakilisha mtazamo wa mataifa mengi ya magharibi.
Akizungumzia sababu za ziara hiyo kwa njia ya Conference call kutoka Washington, Makamu wa Ushauri wa Masuala ya Ulinzi wa Ikulu ya Marekani, Gayle Smith alisema Obama anakwenda Tanzania kwa sababu nchi hiyo ni rafiki mkuu wa Marekani Afrika Mashariki. Alisema Afrika hususan Tanzania, ni moja ya masoko muhimu yanayoibukia ulimwenguni na Marekani lazima iongeze harakati zake barani humo.

0 comments:

Post a Comment