Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday, 2 June 2013

Waislamu TZ waweka msimamo mchakato wa katiba

                                      24Rajab,1434 Hijiriyah/ JUNY 03,2013 Miyladiyah


Waislamu nchini Tanzania wametoa msimamo juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini wakati wa kongamano lililoandaliwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwenye kongamano hilo ambalo masheikh mbalimbali wakiwemo Sheikh Ponda Issa Ponda, Ally Basaleh, Alhaj Mussa Kundecha na Kondo Juma Bungo waliwasilisha mada mbalimbali pamoja na kutangaza maazimio ya kongamano hilo. Moja ya mambo yaliyozungumzwa ni mapendekezo waliyowasilisha kwenye Tume ya Katiba Mpya ambapo walisema iwapo mapendekezo waliyowasilisha hayatazingatiwa  basi Waislamu watatangaza kusimamisha mchakato huo nchi nzima na kufanya maandamano usiku na mchana. Sheikh Ponda amesema kuwa, dhulma na uonevu dhidi ya Waislamu ni mambo ambayo yanayopaswa kukomeshwa nchini humo.
Aidha Sheikh Ponda aliwataka  Waislamu wawe na subira hadi utakapokamilika mchakato wa katiba.

0 comments:

Post a Comment