Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 25 June 2013

'Vita dhidi ya Sheikh wa Kisalafi Lebanon kuendelea'

 
Rais Michel Suleiman wa Lebanon amelaani vikali tangazo la Sheikh wa Kisalafi la kuwataka wafuasi wake kuanzisha vita dhidi ya jeshi la nchi hiyo na kusema halikubaliki. 

Sheikh Ahmad al-Asir ametoa ujumbe huo kwa njia ya video akiwataka wafuasi wake kuendelea kuwashambulia wanajeshi wa Lebanon, kufuatia oparesheni kali ya kumtia mbaroni kiongozi huyo wa Kisalafi mwenye misimamo mikali. 
Rais Michel Suleiman amelaani wito huo wa al-Asir wa kuwachochea Waislamu wa Kisuni wa nchi hiyo kupigana vita na jeshi la nchi hiyo. 
Amesema jeshi la Lebanon linafanya kazi ya kutoa ulinzi kwa makundi mbalimbali ya kisiasa na kimadhehebu nchini humo na kwamba, litakabiliana vikali na mashambulizi yoyote dhidi yake. 
Tangu siku ya Jumapili mji wa Swaida wa kusini mwa Lebanon umekuwa ukishuhudia mapigano makali kati ya wafuasi wa kiongozi huyo wa Kisalafi mwenye misimamo mikali na jeshi la nchi hiyo na kupelekea makumi ya watu kuuwa na wengine wengi kujeruhiwa. Kabla ya hapo wanamgambo wa kiongozi huyo walikishambulia kituo cha upekuzi cha jeshi la nchi hiyo na kuua askari kadhaa.

0 comments:

Post a Comment