Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 25 June 2013

Sudan: Matamshi ya Marekani ni upuuzi

 
Serikali ya Sudan imeyataja matamshi ya afisa mmoja wa Marekani aliyetoa wito wa kushambuliwa kijeshi viwanja vyote vya ndege za kijeshi vya nchi hiyo kuwa ni upuuzi na hayana maana. Hayo yamesemwa leo na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan Abubakar El-Saddiq na kuongeza kuwa mwito wa KenIsaacs, Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Mipango na Mendeleo 'Samaritan's Purse' ya kutaka kushambuliwa viwanja vyote vya ndege za kijeshi vya nchi hiyo kuwa hayana maana yoyote. El-Saddiq  amesema kuwa, madai hayo yanadhihirisha chuki na uadui wa baadhi ya watu wenye misimamo mikali dhidi ya watu na taifa la Sudan. Ameongeza kuwa, mienendo ya watu kama hao, haina nia nyengine ghairi ya kuficha jinai kubwa zinazofanywa na waasi wanaojiita 'Mrengo wa Mapinduzi' dhidi ya raia wasio na hatia wa miji miwili ya Abu Karshola na Um Rawaba. 

Aidha Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ameyalaumu makundi ya watu wenye misimamo mikali nchini Marekani kwa kubadilisha ukweli halisi wa mambo kwa ajili ya kufikia malengo yao machafu. 
Hivi karibuni Ken aliitaka serikali ya Washington kufanya mashambulizi dhidi ya viwanja vya ndege za jeshi la Sudan kwa kile alichodai eti ni kujibu mashambulizi ya serikali ya Khartoum dhidi ya wakazi wa jimbo la Darfur na Blue Nile.

0 comments:

Post a Comment