Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 13 June 2013

NBC KUWAPELEKA WATEJA WAKE HIJJAH KWA KUPITIA HUDUMA YA ISLAMIC WINDOW

                                        


BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kampeni ya miezi miwili na nusu kwa wateja wake wa huduma za kibenki zinazofuata sharia za Kiislamu ili kupata washindi watakaopelekwa Makka kuhiji.
NBC itagharamia safari hiyo ambayo ni sehemu ya ibada iliyolipiwa kila kitu kwa washindi wawili ambao wataondoka Oktoba, mwaka huu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, jijini Dar es Salaam jana Mkuu wa Idara ya Kutoa Huduma za Kibenki kwa Kufuata Sharia za Kiislamu, Yassir Masoud, alisema awamu ya pili ya kampeni hiyo italenga kuwazawadia zaidi wateja wake.
“Tulizindua promosheni hii kwa mara ya kwanza mwaka jana na washindi wetu walifurahia safari zao za kwenda hija na NBC ni benki ya kwanza nchini kuendesha shindano hili na mwaka huu tunatazamia kupeleka wateja wengine kuhiji,” aliongeza.
Awali Mkuu wa Idara ya Hazina ya benki hiyo, Pius Tibazarwa, akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji, aliongeza kuwa uhusiano uliopo kwa benki hiyo na wateja wake ndio ulisababisha kuanzishwa kwa shindano hilo ikiwa ni njia ya kuwashukuru na kuwapongeza.
NBC ilianza kutoa huduma za benki zinazofuata sheria za Kiislamu Mei, 2010 na sasa huduma inayotolewa kuwa ni Akaunti ya Akiba ya Kiislamu, Akaunti ya Hundi ya Kiislamu, Akaunti ya Biashara ya Kiislamu na Akaunti ya Kiislamu kwa Mashirika, nazo hutolewa bila riba.

0 comments:

Post a Comment