Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday 15 June 2013

Masheikh kuumana katika soka Dar Zoo

                             

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, amesema mechi ya soka kati ya Masheikh wa Bakwata na wa Istiqama inayotarajiwa kupigwa kwenye dimba la Dar es Salaam Zoo, Kigamboni kesho, ni mwanzo mzuri kwa viongozi hao wa kidini.
Sadik, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, wakati alipokuwa akikabidhi jezi na mipira kwa viongozi wa timu hizo, na kubainisha kuwa anaamini hiyo ni moja ya njia inayojenga umoja na mshikamano na kulinda afya ya mwili.
Alisema kutokana na mchezo huo, anatarajia itaendelea katika maeneo mengine, lengo likiwa ni kudumisha amani na umoja.
“Kama mnavyojua, mara kadhaa michezo imekuwa ikiwafanya vijana kujiepusha na vitendo vya kihalifu, hivyo nawapongeza kwa kuanzisha mashindano haya,” alisema Sadik.
Kwa upande wake, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salim, alisema mchezo huo wa kirafiki na kudumisha udugu, utarindima kwenye viwanja vya Dar es Salaam Zoo, kuanzia saa 11 jioni.
Aliongeza kuwa malengo ya baadaye, wanakusudia kuandaa mchezo kati yao na maaskofu na wachungaji, kwa madhumuni yale yale ya kudumisha umoja na ushirikiano.
Mwenyekiti wa Istiqama, Swalehe Omar, alisema vifaa hivyo walivyokabidhiwa na gharama nyingine, zimetolewa na Seif Superdoll. 
 

0 comments:

Post a Comment