Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 27 June 2013

Chadema wamjibu Waziri Mkuu

 
Chama cha Maendeleo, Chadema kimeibuka jana bungeni na kusema Serikali inafahamu ukweli wa mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wa chama hicho jijini Arusha.
Chama hicho kimesema Serikali ilitumia kutokuwepo kwao bungeni kupotosha wananchi kuhusu hali halisi juu ya mlipuko wa bomu hilo uliotokea wakati chama hicho kikihitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha, Juni 15, mwaka huu.
Akizungumza kabla ya kuanza kuchangia muswada wa sheria ya fedha ya mwaka 2013/2014, Waziri kivuli wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi wa Chadema, Halima Mdee alisema, “Kabla sijaanza kuchangia Mheshimiwa Spika naomba nianze kwa kuwapa pole wakazi wote wa Arusha kutokana na mlipuko wa bomu uliosababisha watu kupoteza maisha, kwani tangu limetokea tukio hilo leo ndiyo nazungumza kwa mara ya kwanza,”
“Tunazilaani kauli potofu zilizotolewa na Serikali hapa bungeni, Serikali inajua nini kilichotokea Arusha na ilitumia kutokuwepo kwetu kupotosha,” alisema.

 

0 comments:

Post a Comment