Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 11 May 2013

UMOJA WA WANAZUONI WA KIISLAMU TANZANIA WATOA TAMKO KUHUSU MRIPUKO ARUSHAMwenyekiti wa umoja wa wanazuoni Tanzania Sheikh Amrani Kilemile.


Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Hay-atul 'Ulamaa, imewataka Watanzania kutolihusisha suala la hivi karibuni la mripuko wa bomu mjini Arusha na taasisi, kikundi, madhehebu, dini na wala chama chochote na waviachie vyombo husika vifanye uchunguzi wake na hatimae mhusika au wahusika waweze kufikishwa katika vyombo vya kisheria.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania kupitia kwa mwenyekiti wake Sheikh Sulaiman Amran Kilemile pia umewataka Waislamu wote nchini kuwa watulivu na kamwe wasichokozeke na matamshi yanayotolewa na baadhi ya watu au baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vina malengo yao yasiyo bayana.

Vile vile Hay-atul 'Ulamaa imevitaka vyombo hivyo kuweka wazi matokeo ya uchunguzi wa tukio hilo na yanayofanana na hilo kama yale ya Zanzibar, ili kuondoa hisia zinazoweza kusababisha chuki na kudhaniana vibaya kati ya watu wa dini tofauti nchini.

0 comments:

Post a Comment