Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 14 May 2013

Serikali yatangaza mkakati wa kumaliza tatizo la majiSerikali imetangaza mkakati wa kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji katika maeneo ya vijijini na mijini kwa mwaka huu na kusema kuwa mwaka ujao itasambaza huduma hiyo katika vijiji 10 kwa kila wilaya nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, kwenye mkutano wa maji ulioshirikisha washiriki kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.

Profesa Maghembe alisema, serikali itahakikisha mwaka huu asilimia 65 ya Watanzania wanapata huduma ya maji safi na salama na ifikapo mwakani asilimia kati ya 73 hadi 75 watakuwa wamepata huduma hiyo maeneo yao mijini na vijijini.

Aidha, Profesa Maghembe alisema asilimia 42 ya maji yanayozalishwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali yanapotea huku asilimia 16 yakiibiwa na watu wasiokuwa waaminifu jijini Dar es Salaam.

Alifafanua kuwa sera ya maji ya taifa inataka asilimia 80 ya Watanzania vijijini wanaoishi umbali wa mita 400 wawe wamepata huduma ya maji ifikapo mwaka 2025.

Aliongeza kwa sasa ni asilimia 53 ya Watanzania wanaopata huduma ya maji vijijini na asilimia 86 waliopo mijini na kwamba serikali inaweka mkazo kwa maeneo ya vijijini. Kuhusu utunzanji wa vyanzo vya maji, Profesa Maghembe alitaka kila mtu kutunza vyanzo vya maji na kwamba serikali itahakikisha inayatunza mabwawa yote yanayowahudumia wananchi wa vijijini.

Wakizungumza katika mkutano huo kwa nyakati tofauti, baadhi ya washiriki walisema tatizo la maji katika nchi mbalimbali za Afrika ni kybwa na linahitaji mipango ya muda mrefu kukabiliana nalo.

Mwenyekiti wa Mamati ya Ufundi  ya masuala ya maji Afrika (Afwa), Silver Mugisha, akizungumza katika mkutano huo, alisema ili kukabiliana na tatizo la maji lazima kuwe na ofisi za kanda katika kila wilaya kwa ajili ya kuangalia matumizi ya maji yanavyokwenda.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji katika maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo kupanza miti.

Mkutano huo, ulioandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (Dawasa), ulilenga kujadili na kutafuta namna ya kumaliza tatizo la maji mijini na vijijini
.

0 comments:

Post a Comment