Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 18 May 2013

Mifuko yaonywa kunyang’anyana wanachama


Dodoma. Serikali imeita mifuko ya hifadhi ya jamii kutogombea wanachama, badala yake watafute wapya.
Akizungumza katika semina kuhusu mifuko ya Hifadhi ya Jamii jana, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Milton Makongoro alisema mifuko hiyo haina haja ya kugombania wanachama kwani hata waliopo hawatoshelezi.
Dk Makongoro alisema hivi sasa wanachama ni milioni 1.2 sawa na asilimia tatu kati ya sita ya nguvu kazi, ambao ni watu milioni 23.
“Kuna kila sababu ya viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuhakikisha wanatafuta wanachama wapya, badala ya kunyang’anyana wanachama kuna watu wengi ambao hawajajiunga,” alisema Dk Makongoro.
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irine Isaka alisema mamlaka hiyo imeweka utaratibu wa kuhakikisha hakuna urasimu wa huduma za mifuko hiyo.
“Zamani mifuko mingi ilikuwa na urasimu wa kuhudumia wanachama kwa kuweka matabaka, lakini sasa hali hiyo imeisha,” alisema Isaka.
Wakati huohuo, Rais Jakaya Kikwete antafungua maonyesho mifuko hiyo.
 

0 comments:

Post a Comment