Baadhi wananchi wakipanda boda boda maada ya madereva daldal kugoma
Mama na wanawe akiwa juu ya piki piki maarufu kama bodaboda akiwapeleka shule huku askari polisi wakishuhudia usafiri mbadala wa raia manispaa ya Iringa leo asubuhi.
Kazi kweli kweli adha ya usafiri ndiyo hiyo
Baadhi ya abiri wakiwa wamesimama kungojea labda madereva wanaweza kulekeza kamba.Ama kweli"KUFA KUFAANA"Gari aina CENTER likiwa limepakiza abiria baada ya gari za abilria kugoma kufanya kazi yake.
Mgomo wa daladala katika Manispaa ya Iringa umeanza asubuhi hii katika eneo la Mwang'ingo mjini Iringa kwa madereva na wamiliki wa daladala mjini hapa kudai kuchoshwa na manyanyaso ya afisa mpya wa SUMATRA mkoa wa Iringa.
Habari ambazo mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ambazo umezipata zinadai kuwa hatua ya mgomo huo imekuja kutokana na kuchukizwa uamuzi wa Sumatra mkoa wa Iringa kufuta stendi ya posta pamoja na kuzuia daladala kukaa kwa muda eneo la stendi ya daladala ya Miyomboni maeneo ambayo kimsingi walikuwa wakikaa siku zote.
Madereva hao wamesema kuwa leo hawapo tayari kufanya kazi hadi hapo afisa huyo wa Sumatra mkoa wa Iringa atakapofuta maagizo yake ya kuzuia stendi hiyo ya posta na kuruhusu daladala kukaa muda zaidi eneo la Miyomboni .
"Picha na habari ni kwa hisani ya Francis Godwin Blogs"
0 comments:
Post a Comment