Hali ya mvutano inazidi kushuhudiwa katika chama tawala cha Mapinduzi
nhini Tanzania (CCM) ambapo mara hii wabunge wake wamemtaka Rais Jakaya
Kikwete kuwafukuza kazi mawaziri watatu serikalini. Mawaziri wanaotakiwa
kung’olewa ni pamoja na Dakta Shukuru Kawambwa wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Dakta Mathayo David Mathayo wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, na
Dakta Fenella Mukangara wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kama
Rais Kikwete atakubali kuwafuta kazi mawaziri hao, itakuwa mara ya pili
kwake kufanya hivyo ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwezi Mei ambapo
aliamua kuwaengua madarakani baadhi ya mawaziri waliokuwa wakiandamwa
kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo uwajibikaji mbovu na ubadhirifu. Wabunge
hao walichukua msimamo huo hapo jana katika kikao baina yao na Rais
Kikwete kilichokuwa kikitathimini mwenendo wa chama na utendaji wa
wabunge. Wabunge hao walidai kuwa mawaziri hao watatu wamekuwa mzigo kwa
Serikali ya CCM kutokana na utendaji wao kutokuwa wa kuridhisha.
Walisema matunda ya uwepo wa mawaziri hao kwenye wizara husika
hayaonekeni na hivyo kumtaka Rais Kikwete awafute kazi.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment