Wanawake nchini Saudi Arabia wameendeleza maandamano
wakitaka kuachiliwa huru wanawake na watoto ambao wanashikiliwa katika
jela za nchi hiyo kwa sababu tu ya kuupinga utawala wa kifalme wa Aal
Saud.
Katika maandamano ya hivi karibuni, siku ya Jumamosi
wanawake waliandamana katika mji wa Buraydah wakidai haki zao na kutaka
wafungwa wa kisiasa waachiliwe huru. Kwa mujibu wa Jumuiya ya Haki za
Kisiasa na Kiraia Saudi Arabia, takribani wafungwa 30 elfu wa kisiasa
wanashikiliwa katika jela za Ufalme wa Aal Saud. Wafungwa wengi
wanashikiliwa gerezani bila kufunguliwa mashtaka huku wengine
wakiendelea kuzuiliwa pamoja na kuwa vifungo vyao vimemalizika.
Maandamano ya kudai haki hivi karibuni yalifanyika katika mji mtakatifu
wa Makkah. Aidha maandamano kama hayo yamekuwa yakifanyika katika eneo
la mashariki mwa nchi hiyo pamoja na mji mkuu Riyadh. Walio wengi Saudi
Arabia wanataka uhuru wa kuwachagua viongozi wao pamoja na kukomeshwa
dhulma na ubaguzi nchini humo. Maandamano ya wananchi huko Saudia
yanafanyika katika fremu ya Mwamko wa Kiislamu ambao umekuwa
ukishuhudiwa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Ikumbukwe kuwa Saudi
Arabia ni muitifaki mkubwa wa Marekani katika eneo
0 comments:
Post a Comment