Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 18 October 2012

Walibya 11 wauawa katika mapigano Bani Walid

Watu wasiopungua 11 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya waasi wa zamani wa Libya wenye mfungamano na jeshi kushambulia mji wa Bani Walid.
Massud al Waer afisa wa eneo hilo amesema mji huo umeshambuliwa mara tatu na kwamba makumi ya wakazi wake wamejeruhiwa. Hata hivyo duru za jeshi la Libya zimesema kuwa hazijatoa amri yoyote ya kushambuliwa mji huo.
Mashambulizi hayo yametokea ukiwa umepita mwaka mmoja tangu mji huo ulioko umbali wa kilometa 170 kusini mashariki mwa mji mkuu Tripoli ukombolewe kutoka katika udhibiti wa vikosi vilivyokuwa vikimuunga mkono dikteta wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi. Hata hivyo Walibya wengi wanaamini kuwa mji wa Bani Walid bado ni ngome ya wapiganaji wa zamani wa Gaddafi na magenge ya watenda jinai.

0 comments:

Post a Comment