Serikali ya Guinea Conakry na vyama
vya upinzani wameafikiana juu ya kufanyika uchaguzi wa Bunge uliocheleweshwa
kwa muda mrefu, mwishoni mwa mwezi Septemba, ili kuhitimisha kipindi cha mpito.
Mauktar Diallo ambaye ni mmoja kati
ya viongozi wa upinzani amesema, wamefikia makubaliano hayo na kwamba ana
matumaini jamii ya kimataifa pia itahakikisha yanatekelezwa. Diallo ameongeza
kwamba, makubaliano hayo yanamaanisha kuwa, uchaguzi wa Bunge utafanyika baada
ya siku 83 tarehe 29 Septemba mwaka huu.
Awali uchaguzi huo ulipangwa
kufanyika Juni 30 lakini uliakhirishwa baada ya wimbi la maandamano ya
wapinzani waliokuwa wakimtuhumu Rais Alpha Conde kuwa ana mpango wa kuiba kura.
0 comments:
Post a Comment