Mahakama ya Uturuki imefuta mpango
wa serikali wa kubomolewa bustani iliyo karibu na Medani ya Taksim mjini
Istanbul, suala lililozusha maandamano ya kupinga serikali nchini humo.
Uamuzi wa mahakama hiyo unaonekana
kuwa pigo kwa Waziri Mkuu Racep Tayyip Erdogan aliyekuwa aking'ang'ania mpango
huo, na unaonekana kuwa ushindi kwa wapinzani waliokuwa wakiupinga.
Tangu Mei 31 Istanbul imekuwa
ikishuhudia maandamano ya kupinga serikali huku polisi wakikabiliana na
waandamanaji waliokuwa wamepiga kambi katika Medani ya Taksim kupinga uamuzi wa
kubomolewa bustani ya Gezi. Bustani hiyo imezoeleka kuwa eneo la mijumuiko,
mikusanyiko na maandamano na pia kivutio cha watalii huku ikiwa ni sehemu pekee
ya kijani ya umma iliyobakia kwenye mji wa Istanbul na serikali ilitaka
kuibomoa kujenga maduka.
0 comments:
Post a Comment