Mustapha Barghouthi mmoja kati ya
viongozi wa mapambano wa Palestina amejeruhiwa katika shambulizi lililofanywa
na askari wa Israel.
Barghouthi alijeruhiwa jana katika
shambulizi lililofanywa na jeshi la utawala wa Kizayauni dhidi ya maandamano ya
Wapalestina huko katikati ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwenye mji wa
Beitin.
Kiongozi huyo wa muqawamah wa Palestina amesema, askari wa Israel pia
wamewajeruhi makumi ya Wapalestina wengine waliotoka katika miji ya Jenin, al
Khalil, Nablus, Ramallah na Tulkarem kwenye tukio hilo. Barghouth amesema,
matumizi ya mabavu dhidi ya maandamano ya amani hayatawazuia Wapalestina
kupinga ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zao.
Hatua ya Israel ya kuendelea kupanua
ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina
inazozikalia kwa amabavu imekuwa kikwazo kikuu cha kupatikana amani Mashariki
ya Kati.
Umoja wa Mataifa na nchi nyingi duniani zinasema kwamba, vitongoji
hivyo vya Israel si halala kwa kwamba vinajengwa katika ardhi za Palestina
zilizoporwa katika vita vya mwaka 1967 na Mkataba wa Geneva unazuia kujenga
katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
0 comments:
Post a Comment