Wakati unakaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa mara ya kwanza kabisa kanali ya 4 ya televisheni ya nchini Uingereza itakuwa ikirusha hewani moja kwa moja adhana ya sala ya asubuhi.
Justine Bower mkurugenzi wa masuala
ya umma wa kanali ya 4 ya televisheni ya nchi hiyo amesema kuwa, kanali hiyo
itakuwa ikirusha moja kwa moja adhana ya asubuhi kwa ajili ya wananchi wa
Uingereza. Ameongeza kuwa, waumini wa dini ya Kiislamu wapatao milioni mbili na
laki nane nchini humo wataanza mfunguo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani siku
chache zijazo. Bower amesema kuwa kanali hiyo pia itakuwa ikirusha hewani
adhana kupitia mtandao wa kanali hiyo.
Alipoulizwa wamejiandaa vipi
kukabiliana na ukosoaji kwa hatua hiyo, Justine Bower amesema kuwa, karibu
asilimia 5 ya wananchi wa nchi hiyo wako katika pirika za kuukaribisha mwezi
mtukufu wa Ramadhani. Amesema kuwa, mwezi wa Ramadhani hufungwa na waumini wa
dini ya Kiislamu kila mwaka, na nitawashangaa watu watakaostaajabishwa na uwepo
wa utambulisho huo wa kidini.
0 comments:
Post a Comment