Rais Barack
Obama wa Marekani, anatarajia kuwasili saa nane mchana nchini Tanzani kwa ziara
rasmi ya siku mbili. Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zilizotembelewa
tayari na Rais Obama. Hata hivyo wananchi wengi wa Tanzania wamelalamikia
safari hiyo, kutokana na kuzorota shughuli zao za kijamii kwa muda wa wiki moja
sasa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Obama anayeongozana na familia yake anatarajiwa
kupokelewa jijini Dar es Salaam na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete na
baadaye kwenda Ikulu kwa mazungumzo rasmi. Hapo juzi polisi nchini Afrika
Kusini walipambana na waandamanaji waliokuwa na hasira ambao waliteketeza moto
picha za rais huyo wa Marekani alipokuwa safarini nchini humo. Waandamanaji hao
pia waliteketeza moto bendera za Marekani katika maandamano hayo yaliyofanyika
nje ya Chuo Kikuu cha Johannesburg, tawi la Soweto, sehemu ambayo Obama
aliwahutubia wanafunzi. Akiwa nchini Senegal Rais Macky Sall wa nchi hiyo
alimwambia kinagaubaga Obama kuwa, nchi yake haiko tayari kuruhusu ushoga na
maingiliano ya ngono kati ya watu wa jinsia moja.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment