Jeshi la Misri limetangaza kuwa, taarifa
iliyotolewa jana kwa makundi ya kisiasa ya kuyataka yafikie mwafaka,
haina maana ya kutaka kufanya mapinduzi ya kijeshi nchini humo.
Jeshi la Misri limeeleza kuwa, taarifa hiyo
imetolewa kwa lengo la kuyashinikiza makundi ya kisiasa na wanasiasa
nchini humo kufikia mwafaka na serikali ya Cairo. Taarifa hiyo imeeleza kuwa,
iwapo wanasiasa wa Misri watashindwa kufikia mwafaka na kutekeleza matakwa ya
wananchi katika kipindi cha masaa 48 yajayo, litalazimika kuingilia kati kwa
shabaha ya kutatua mgogoro huo.
Wakati huohuo, masaa machache baada ya jeshi
kutoa muda wa masaa 48 ya kutatuliwa mgogoro wa Misri, Waziri wa Mambo ya Nchi
za Nje wa Misri Muhammad Kamil Amr ametangaza kujiuzulu, baada ya kushadidi
maandamano ya wapinzani wa Rais Morsi. Hadi sasa mawaziri 10 na magavana watatu
wa serikali ya Misri wameshajiuzulu. Vilevile mshauri wa masuala ya kijeshi wa
Rais Morsi naye alitangaza kujiuzulu hapo jana.
0 comments:
Post a Comment