Rais Bashar al Assad wa Syria amepiga
marufuku utumiwaji watoto kwenye operesheni za kijeshi na kusisitiza kuwa
watakaopatikana na hatia ya kuwatumia watoto hao watakabiliwa na adhabu kali ya
kifungo jela.
Rais Assad ameongeza kuwa, mtu yeyote
atakayethubutu kuwashirikisha vijana walio na umri wa chini ya miaka 18 kwenye
oparesheni za kijeshi na masuala yanayofungamana nayo kama kubeba silaha, zana
za kijeshi na kutega mada za milipuko kwenye vituo vya ukaguzi na maeneo
mengineyo watakabiliwa na kifungo cha kuanzia mwaka mmoja hadi 10 jela na
kulipa faini ya lira milioni tatu.
Rais wa Syria ameongeza kuwa, adhabu ya
kifungo cha maisha itatolewa kwa watu ambao watapatikana na hatia ya
kuwalazimisha watoto kubeba mada za milipuko na iwapo watoto hao watauawa, basi
wahusika watakabiliwa na adhabu ya kifo.
0 comments:
Post a Comment