Rais Barack Obama wa Marekani amezitaka nchi
zinazopakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuacha mara moja uungaji mkono
wao kwa makundi ya waasi nchini humo.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa
habari Ikulu mjini Dar es Salaam akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete wa
Tanzania, Rais Obama pia amemtaka Rais Joseph Kabila wa Kongo kupanga mikakati
ya haraka ya kulikarabati na kulijenga upya jeshi la nchi hiyo. Rais wa
Marekani ameongeza kuwa, wananchi wa Kongo wanahitaji kupewa fursa, kwani
mapigano ya miaka kadhaa nchini humo yamewanyima fursa ya kupiga hatua za
kimaendeleo.
Obama amesema kuwa, makubaliano ya amani
yaliyotiwa saini mwezi Februari mwaka huu yenye lengo la kurejesha amani na
utulivu mashariki mwa Kongo hayapaswi kubaki kwenye makaratasi bali yanabidi
kufanyiwa kazi. Rais Barack Obama wa Marekani aliwasili Tanzania jana alasiri
kwa ziara ya siku mbili, baada ya kuzitembelea nchi za Senegal na Afrika
Kusini.
0 comments:
Post a Comment