Mahakama ya Strasbourg nchini Ufaransa
imemuhukumu adhabu ya kifungo cha miezi mitatu jela na faini ya euro 1,000 raia
wa nchi hiyo aliyepatikana na hatia ya kukivunjia heshima kitabu kitakatifu cha
Mwenyezi Mungu, Qurani Tukufu.
Mahakama hiyo imeeleza kuwa, mhalifu huyo
alikuwa akitafutwa na vyombo vya sheria kwa kosa la kuteketeza moto na
kukivunjia heshima kitabu hicho kitakatifu.
Vitendo vya chuki na uadui dhidi ya dini
tukufu ya Kiislamu vimekuwa vikishamiri kila uchao nchini Ufaransa. Miongoni
mwa vitendo hivyo ni kushambuliwa wanawake wanaovaa hijabu ya Kiislamu katika
eneo la Val-d'Oise kaskazini mwa Ufaransa.
Hivi karibuni Baraza la Utamaduni la Waislamu
nchini Ufaransa CFCM lilitangaza kuwa, kuanza mwaka huu wa 2013, zaidi ya
misikiti 10 imeshambuliwa na kuvunjiwa heshima na Wafaransa wenye chuki na
uadui dhidi ya Uislamu.
0 comments:
Post a Comment