Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 25 June 2013

Mtawala wa Qatar amuachia mwanawe utawala

  Mtawala wa Qatar, Sheikh Hamad bin Khalifa Aal Thani ameondoka rasmi madarakani na kumuachua mamlaka manawe Sheikh Tamim bin Hamad Aal Thani.
Amiri huyo mwenye umri wa miaka 61, ambaye aliingia madarakani mwaka 1995 baada ya kumpindua baba yake, sasa amemuachia madaraka mwanawe mwenye umri wa miaka 33 katika hafla iliyofanyika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Doha.
Akizungumza kwa njia ya televisheni Sheikh Hamad bin Khalifa Aal Thani alidai kwamba, uamuzi wake huo unalenga kuachia kizazi cha vijana fursa ya kuongoza.
Duru zinaarifu kuwa, baraza la mawaziri pia litabadilishwa ili vijana wachukue nyadhifa muhimu. Weledi wa mambo wanasema, mtawala huyo wa Qatar amejiuzulu kufuatia mashinikizo ya Marekani.
Mfalme mpya wa Qatar, sawa na baba yake, anatazamiwa kuendelea kuwa kibaraka wa Marekani katika eneo hili la Mashariki ya Kati.
Itibari ya Qatar imeharibika kimataifa hasa kati ya Waislamu kutokana na kujihusisha nchi hiyo ndogo na uungaji mkono kwa magaidi wanaotaka kuiangusha serikali halali ya nchini Syria, na wakati huo huo kufanya urafiki wa wazi na utawala wa Kizayuni wa Israel.

0 comments:

Post a Comment