Serikali ya
Sudan imeyataja matamshi ya afisa mmoja wa Marekani aliyetoa wito wa
kushambuliwa kijeshi viwanja vyote vya ndege za kijeshi vya nchi hiyo kuwa ni
upuuzi na hayana maana. Hayo yamesemwa leo na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje
ya Sudan Abubakar El-Saddiq na kuongeza kuwa mwito wa KenIsaacs, Naibu
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Mipango na Mendeleo 'Samaritan's Purse'
ya kutaka kushambuliwa viwanja vyote vya ndege za kijeshi vya nchi hiyo kuwa
hayana maana yoyote. El-Saddiq amesema kuwa, madai hayo yanadhihirisha
chuki na uadui wa baadhi ya watu wenye misimamo mikali dhidi ya watu na taifa
la Sudan. Ameongeza kuwa, mienendo ya watu kama hao, haina nia nyengine ghairi
ya kuficha jinai kubwa zinazofanywa na waasi wanaojiita 'Mrengo wa Mapinduzi'
dhidi ya raia wasio na hatia wa miji miwili ya Abu Karshola na Um Rawaba.
Aidha
Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ameyalaumu makundi ya watu
wenye misimamo mikali nchini Marekani kwa kubadilisha ukweli halisi wa mambo
kwa ajili ya kufikia malengo yao machafu.
Hivi karibuni Ken aliitaka serikali
ya Washington kufanya mashambulizi dhidi ya viwanja vya ndege za jeshi la Sudan
kwa kile alichodai eti ni kujibu mashambulizi ya serikali ya Khartoum dhidi ya
wakazi wa jimbo la Darfur na Blue Nile.
0 comments:
Post a Comment