Rais Michel
Suleiman wa Lebanon amelaani vikali tangazo la Sheikh wa Kisalafi la kuwataka
wafuasi wake kuanzisha vita dhidi ya jeshi la nchi hiyo na kusema halikubaliki.
Sheikh Ahmad al-Asir ametoa ujumbe huo kwa njia ya video akiwataka wafuasi wake
kuendelea kuwashambulia wanajeshi wa Lebanon, kufuatia oparesheni kali ya
kumtia mbaroni kiongozi huyo wa Kisalafi mwenye misimamo mikali.
Rais Michel
Suleiman amelaani wito huo wa al-Asir wa kuwachochea Waislamu wa Kisuni wa nchi
hiyo kupigana vita na jeshi la nchi hiyo.
Amesema jeshi la Lebanon linafanya
kazi ya kutoa ulinzi kwa makundi mbalimbali ya kisiasa na kimadhehebu nchini
humo na kwamba, litakabiliana vikali na mashambulizi yoyote dhidi yake.
Tangu
siku ya Jumapili mji wa Swaida wa kusini mwa Lebanon umekuwa ukishuhudia
mapigano makali kati ya wafuasi wa kiongozi huyo wa Kisalafi mwenye misimamo
mikali na jeshi la nchi hiyo na kupelekea makumi ya watu kuuwa na wengine wengi
kujeruhiwa. Kabla ya hapo wanamgambo wa kiongozi huyo walikishambulia kituo cha
upekuzi cha jeshi la nchi hiyo na kuua askari kadhaa.
0 comments:
Post a Comment