Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 25 June 2013

Kifaa maalum kutumika kufuatilia mapato ya simu




 
Kilio cha muda mrefu cha wabunge kulalamikia ukwepaji wa kodi unaofanywa na makampuni ya simu za mikononi, hatimaye kimepatiwa ufumbuzi baada ya serikali kununua kifaa maalum za kufuatilia mfumo wa mapato yatokanayo na huduma za simu.
Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene, akijibu hoja za wabunge mbalimbali waliochangia Bajeti ya Serikali, alisema jana kuwa kifaa hicho kitafungwa mwezi ujao na kuanza kutumika.

Alisema kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), seriakali itaweza sasa kudhibiti na kupata mapato stahiki kutoka kwa makampuni hayo.

Kifaa hicho alisema kuwa ni Telecommunications Traffic Monitoring System.

Kumekuwa na kilio cha muda mrefu toka kwa wabunge na wananchi wakilalamikia makampuni ya simu kushindwa kulipa kodi stahiki na kuikosesha serikali kiasi kikubwa cha fedha kwa kuwa haikuwa rahisi kujua mapato halisi ambayo kampuni hayo yalikuwa yakipata.

Alisema kifaa hicho ambacho kitatumika kupima pia ubora wa huduma za simu na kuanzisha mifumo mbalimbali ya simu, pamoja na mambo mengine kitasaidia kujua kiasi cha kodi ambacho serikali inatakiwa kupata kutoka mapato halisi ya simu


0 comments:

Post a Comment