Sikiliza Live
Friday, 11 January 2013
MFALME WA SAUDI ATEUA WANAWAKE KUINGIA BUNGENI
Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia, kwa mara ya
kwanza ameteua wanawake 30 kuingia katika bunge
la nchi hiyo, kwa mujibu wa amri ya kifalme
iliyochapishwa na shirika la habari la nchi hiyo SPA.
Amri hiyo inawapa wanawake jumla ya nafasi moja
ya tano katika baraza la Shura, ambalo ndilo bunge
rasmi la taifa hilo linaloongoza kwa uzalishaji wa
mafuta. Wajumbe wote 150 wa baraza hilo huteuliwa
na mfalme. Mwaka 2011 Abdullah aliahidi
kuwaruhusu wanawake kugombea na kupiga kura
katika uchaguzi wa serikali za mitaa kama sehemu
ya mageuzi. Uchaguzi ujao utafanyika mwaka 2015.
Saudi Arabia ndiyo nchi pekee ya Kiislamu
isiyoruhusu wanawake kupiga kura. Wanawake wa
Saudi Arabia hawaruhusiwi pia kuendesha magari,
na hawawezi kusafiri bila ya kusindikizwa na mlinzi
wa kiume au wawe na umri wa zaidi ya miaka 45.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment