Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Friday, 11 January 2013

MAJESHI YA MAREKANI KUACHA MAPIGANO AFGHANISTAN

Rais wa Marekani Barack Obama na mwenzake wa Afghanistan Hamid Karzai, wamekubaliana kuwa vikosi vya Marekani nchini Afghanistan vitamaliza operesheni zake nyingi za mapambano mwishoni mwa  mwaka  huu. Viongozi hao walitoa taarifa ya pamoja katika ikulu ya Marekani White House jana Ijumaa, kuhusu mustakabali wa vikosi vya Marekani nchini Afghanistan. Wanajeshi hao wanatarajiwa kuchukuwa jukumu la usaidizi, miezi michache mapema kuliko ilivyopangwa. Obama na Karazai pia waliunga mkono kufanyika kwa mazungumzo mjini Doha, Qatar, kati ya serikali ya Afghanistan na viongozi wa kundi la Taliban. Zaidi ya wanajeshi 66,000 wa Marekani walioko Afghanistan wataondoka mwaka 2014.

0 comments:

Post a Comment