Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Friday, 11 January 2013

CAR, WAASI WAFIKIA MAKUBALIANO

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na waasi wamekubaliana jana Ijumaa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano. Makubaliano hayo yaliyosainiwa katika mji mkuu wa Gabon, Libreville baada ya siku tatu za upatanishi wa mataifa jirani, yameondoa kitisho kikubwa zaidi dhidi ya utawala wa muongo mmoja wa rais Francois Bozize, katika koloni hilo la zamani la Ufaransa. Msemaji wa muungano wa waasi wa Seleka Eric Massi alisema makubaliano hayo ni mazuri kwa mustakabali wa taifa, lakini alionya kuwa mapigano yanaweza kuripuka tena endapo serikali itashindwa kutekeleza matakwa ya waasi yaliyojumlishwa katika makubaliano hayo. Madai hayo ni pamoja na kuachiwa kwa wafungwa wote wa kisiasa, na kuondoa vikosi vyote vya kigeni vilivyoingizwa kusaidiana na serikali. Makubaliano hayo yalitaka kuundwa kwa serikali ya muungano ambayo itakuwa na waziri mkuu kutoka upinzani, na kufanyika kwa uchaguzi wa bunge jipya ndani ya miezi 12.

0 comments:

Post a Comment