Sikiliza Live
Friday, 23 November 2012
Rais Muhammad Mursi akubali masharti ya Wazayuni
Rais Muhammad Mursi wa Misri amekubali mapendekezo yaliyotolewa na
viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel la kuwekwa mifumo ya
elektroniki itakayolinda mipaka, ikiwa ni miongoni mwa masharti ya
kukubali kusitisha mapigano kati ya utawala huo ghasibu na Wapalestina
wa eneo la Ukanda wa Gaza. Taarifa zinasema kuwa, Hosni Mubarak dikteta
wa zamani aliyeng'olewa madarakani nchini humo, kwa muda wa miongo
mitatu alikuwa akipinga vikali pendekezo hilo kwa kusema kuwa
linainyima Misri haki ya kudhibiti kikamilifu mipaka yake. Duru za
habari kutoka Tel Aviv zinasema kuwa, katika hali ambayo Rais Mursi
amekubali pendekezo hilo, amma taasisi na asasi za kisiasa na kiusalama
za Israel haziamini kwamba kiongozi huyo wa Misri ataweza kutekeleza
kikamilifu ahadi yake hiyo. Iwapo mifumo hiyo ya elektroniki itawekwa
kwenye mipaka ya Misri na utawala wa Israel, majeshi ya utawala huo
ghasibu yataweza kukusanya taarifa zote za kiusalama mpakani na kuzituma
makao makuu ya jeshi la Israel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 comments:
Post a Comment