Sikiliza Live
Friday, 23 November 2012
Mufti Mkuu wa Tanzania alaani jinai za Israel, Gaza
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Bin Shaaban Simba amelaaani jinai za
utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza Palestina ambapo makumi ya
wanawake, watoto, wazee na vijana wasio na hatia wameuawa hivi karibuni
kufuatia hujuma na amshambulio ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza. Mufti
Simba amesema, analaani mauaji yanayofanywa na Israel dhidi ya wananchi
wa Palestina. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mufti Mkuu wa
Tanzania amesema, anatoa wito kwa viongozi wa kitaifa na wale wa
kimataifa, likiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kutafuta
haraka suluhisho la kudumu la kadhia ya Palestina. Amesema, Baraza Kuu
la Waislamu nchini Tanzania BAKWATA siku zote limekuwa na itaendelea
kuwa mstari wa mbele kuunga mkono harakati za Wapalestina za kupigania
haki zao za kimsingi ikiwemo ya kuwa na nchi yao huru ya Palestina.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 comments:
Post a Comment