Sikiliza Live
Thursday, 29 November 2012
Palestina yatambuliwa na UN
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana limeipandisha hadhi Palestina kwa wingi
wa kura kuwa kama taifa lisilo mwanachama wa umoja huo. Rais wa Palestina
Mahmoud Abbas ameshinda ombi lake aliloliwasilisha la kupewa hadhi hiyo.
Abbas ameungwa mkono na nchi 138 wanachama wa baraza hilo lenye jumla
ya wanachama 193. Nchi wanachama 41 wa baraza hilo hawakupiga kura
huku nchi tisa zikipiga kura ya hapana, ikiwemo Marekani na Israeli. Ushindi
huo wa Palestina umeonyesha kushindwa kidiplomasia kwa Marekani na
Israeli ambazo ziliungwa mkono na mataifa machache kupinga hatua ya
kuipandisha hadhi Palestina kutoka kuwa kama mtazamaji kwenye Umoja wa
Mataifa na sasa kuwa kama taifa lisilo mwanachama wa umoja huo kama
ilivyo kwa Vatican. Abbas amesema ushindi huo umepokewa kwa shangwe
katika mji wa Ramallah, kwenye Ukingo wa Magharibi, ambapo watu
wamejitokeza mitaani kushangilia. Hata hivyo, ofisi ya Waziri Mkuu wa Israeli,
Benjamin Netanyahu imelaani vikali hatua hiyo kwa kile ilichokiita hotuba ya
sumu kutoka kwa kiongozi huyo wa Palestina ambaye ameishutumu Israeli
kutokana na propaganda za uongo. Netanyahu amesema hayo siyo
matamshi ya kutolewa na mtu anayetaka amani na amesisitiza kwamba amani
ya mashariki ya kati itafikiwa kwa mazungumzo ya ana kwa ana baina ya
Palestina na Israeli.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 comments:
Post a Comment