Sikiliza Live
Friday, 16 November 2012
Qandil atembelea Ghaza kuunga mkono Wapalestina
Waziri Mkuu wa Misri, Hisham Qandil mapema leo amefanya ziara fupi
katika ukanda wa Ghaza kwa lengo la kuonyesha uungaji mkono wake kwa
wananchi wa Palestina hususan katika ukanda huo wanaoendelea kukabiliwa
na mashambulizi ya utawala haramu wa Israel kwa siku ya tatu mfululizo.
Qandil amelaani jinai hizo za Wazayuni dhidi ya wananchi wasio na hatia
wa eneo la Ghaza na kusisitiza kuwa serikali ya Cairo haitafumbia macho
mauaji hayo. Qandil ametembelea majeruhi wa Kipalestina katika hospitali
moja huko Ghaza. Huku hayo yakijiri, Jumuiya ya Nchi zisizofungamana na
Siasa za Upande Wowote NAM imetoa taarifa ya kulaani mashambulizi ya
Israel huko Ghaza na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
kuchukua hatua za dharura kukomesha unyama huo wa Wazayuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 comments:
Post a Comment