Sikiliza Live
Thursday, 15 November 2012
Mashambulizi ya Israeli huko Gaza hayakubaliki
Rais Muhammad Mursi wa Misri amesema kuwa, mashambulizi yanayofanywa na
majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza,
hayakubaliki hata kidogo. Rais Mursi amechukua uamuzi wa kumrejesha
nyumbani balozi wa nchi hiyo aliyeko Tel Aviv, ikiwa ni radiamali ya
kulalamikia unyama na ukatili unaofanywa na majeshi ya Israel dhidi ya
wananchi wa Palestina wa eneo la Ukanda wa Gaza. Aidha Rais Mursi
ametaka kiitishwe kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa kwa shabaha ya kujadili mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza.
Rais wa Misri amesisitiza kuwa, kushadidishwa mashambulizi hayo
kutapelekea eneo la Mashariki ya Kati kukosa uthabiti. Kwa upande
mwengine, Misri imefungua kivuko cha ardhini cha Rafah, baada ya
kushadidi mashambulizi ya Wazayuni. Taarifa zinasema kuwa, kivuko hicho
kimefunguliwa ili kuwaruhusu majeruhi wa Kipalestina kupelekwa kwenye
hospitali ya al A'rish iliyoko upande wa Sinai ya Kaskazini ndani ya
ardhi ya Misri. Inafaa kuashiria hapa kuwa, mashambulizi ya Wazayuni
katika eneo hilo la Wapalestina yamesababisha watu wasiopungua 20 kuuawa
shahidi na wengine zaidi ya 125 kujeruhiwa katika kipindi cha masaa 24
yaliyopita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 comments:
Post a Comment