Bila shaka wengi wetu tumesoma au kusikia kuhusiana na
Hijra(kuhama)kwa mtume na maswahaba zake k...
utoka Makka na kuelekea Madina.
Hapa ndipo ilipo anza tarehe ya kiislamu.
Katika safari hii ya mtume kuna mazingatio mengi sana,
Haya hapa ni baadhi ya mazingatio tunayo yapata katika safari hiyo:
1:Mazingatio ya uhamaji:
Mwenyezi Mungu alitoa idhini kwa mtume wake na
waumini kuhama toka Maka kutokana na Madhara na mateso mbali mbali
waliyo kuwa wakiyapata kutoka kwa makafiri wa kikurayshi.Katika haya madhara ilikuwa ni kuwazuia waislamu
Kuisimamisha dini yao,wakateshwa na kuadhibiwa vikali.
Ndio Allah alipo toa idhini hii ya kuhama kwa mtume na maswahaba wake
wa elekea sehemu watakayokuwa na uhuru wa kumuabudu Allah na kusimamisha uislamu pasina ya bughdha zozote.
Maana ya kuhama kisheria haiishii katika kutoka sehemu moja na kuelekea sehemu nyingine,kutoka katika mji mmoja na kuelekea katika mji mwingine.Bali ni kulihama kila lile lililo
katazwa na Mwenyezi Mungu ili mja maisha yake yote
yawe ni kwa ajili ya Allah.
=Kuyahama madhambi na maasi,kuyahama matamaniyo
yenye kumpeleka mja kumuasi Allah,kuzihama sehemu zenye kufanyika
maovu na kuzihama sehemu za maovu, kama vile madangulo bar vilabu na mengineyo.
Kuhama kutoka katika ufinyo wa dunia na kuelekea katika upana wa akhera,hali itakayo mpelekea mja aishi hali ya kujua kuwa hapa duniani si ndio mwisho wa maisha, bali kesho akhera kuna maisha ya milele na milele.
2:Subira na yakini ni njia ya kunusuriwa na kumakinishwa katika ardhi:
Baada ya miaka 13 ya kubanwa kuteswa na kudhulumiwa,muda ambao alio uishi mtume na maswahaba zake kule Makka,Allah akawaandalia waislamu
Ardhi nzuri na kuingiza imani katika nyoyo za Maanswari na kuanza mrorongo wa nusra na kumakinishwa(kuthibitishwa)
katika ardhi kwa wale watu walio kuwa na subira na yakini yaani mtume na maswahaba zake.
قال الله تعالي:( إنا لننصر رسلنا والذين آمنوا في الحياة الدنيا ويوم الأشهاد )سورة غافر:51
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
(Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama mashahidi) Surat Ghafir:51
Hakika njia ya kushikamana na dini ya Allah na kuwalingania watu juu ya dini hii ya kweli,ni njia iliyo zungukwa na mitihani mbali mbali na mambo ya kuchukiza
Na baadhi ya nyakati huwa ni mambo yenye kukatisha tama.
Lakini kwa mwenye kusubiri na kuthibiti basi huyo ndiye atakaye faulu kuneemeka na kupata furaha ya kweli ya maisha.
(والله غالب على أمره ولكن أكثر الناس لا يعلمون)
سورة يوسف:21
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
(Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui)Surat Yusuf:21
3:Mazingatio ya kumtegemea Allah na kushikamana na kamba(dini) yake:
Kwa hakika safari ya kuhama kwa mtume ilikuwa
Ni safari iliyo zungukwa na hatari na umauti.Kwani makafiri baada ya kusikia habari za kuhama kwa mtume -rehema na amani ziwe juu yake- waliizunguka nyumba ya mtume wakiwa na mapanga wakihitaji kumuua mtume wa Allah,
Walikuwa washajiweka tayali wakisubiri atoke tu ili waweze mmaliza.
Lakini kwa uwezo wake Allah alimsalimisha mtume wake na kumtoa salama pasina ya makafiri kumuona.
Na pindi alipo ondoka nyumbani kwake na kwenda kujificha pangoni,makafiri wamefika mpaka katika mlango wa pango kiasi kwamba mmoja wao akiangalia chini tuu basi atamuona mtume na Abubakari,lakini Allah akawanusuru mtume na Abu bakari.
Na pindi Suraka alipo kuwa akimfukuza mtume mpaka akawa kamkaribia kabisa akawa akisikia kisomo cha mtume,lakini ghafla miguu ya farasi wa Suraka inadidimia chini tena ni sehemu ya mawe! Kisha baada ya hapo linatimuka vumbi kubwa na kumfanya Suraka asimuone mtume.
Mtume katika hali zote hizi alikuwa ni mwenye kuthibiti na kumtegemea Allah na kuwa na yakini Naye.
Kwani yeye ajua ya kwamba maadamu Allah kaniahidi nusra basi ataninusuru tu.
Hivi ndivyo inavyo kuwa hali ya muumini,vyovyote vile yatakapo mzidia matatizo na mitihani basi hateteleki kwani yeye ajua ahadi ya Allah mbele ya mawalii wake( waja wenye kumuamini Allah na kumtii), na anajua ya kwamba baada ya dhiki ni faraja.
قال الله تعالي:
( فإن مع العسر يسري .إن مع العسر يسرا)سورة الشرح:5-6
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
(Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi. Hakika pamoja na uzito upo wepesi)
Surat Asharh:5-6
Allah kasema hakika pamoja na uzito upo wepesi licha ya kwamba kimoja hukitangulia kingine,yaani waweza anza uzito kisha ukaja wepesi,lakini Allah kasema pamoja na uzito upo wepesi kuashiria ya kwamba penye uzito pasi wepesi huja haraka sana mpaka viwili hivyo vikafanywa kama vipo pamoja.
Kwa hiyo mja pindi utapopatwa na uzito juu ya suala lolote la kheri basi usikate tama bali zidi chukua sababu na kusubiri faraja ya Allah ambayo ipo karibu nawe.
4:Mazingatio juu ya miujiza ya Allah:
Je mshawahi muona mtu dhaifu aliye zungukwa na maadui wenye silaha kali,kisha mtu huyu dhaifu anatoka na kuwamwagia maadui mchanga nyusoni mwao na hawamuoni???!!!
Je mshawahi muona buibui akitanda utando wake katika mlango wa pango kwa muda wa saa chache tu???!!!
Je mshawahi ona maadui wanamtafuta adui yao na kupanda mpaka mlimani na kusimama katika mlango wa pango pasina ya hata mmoja wao kujaribu kuangalia kilichomo katika pango???!!!
Je mshawahi muona farasi akikimbia katika ardhi ngumu kisha miguu yake yadidimia kama vile anatembea katika tope?na kutimuka vumbi kubwa mpaka mbele kukawa hakuonekani???!!!
Je mshawahi muona mbuzi mdogo ambaye hajazaa yakibubujika toka katika kiwele chake maziwa ya kutosheleza idadi ya watu wengi???!!!
Hakika miujiza hii ni dalili tosha juu ya uwezo wa Allah,
Na iwapo kama Allah atataka kuwanusuru waumini basi mizani yote hugeuzwa na mambo kwenda tofauti na inavyo fahamika kwa watu wengi.
( قال الله تعالي(إنما أمره إذا أراد شيئاً أن يقول له كن فيكون
سورة يس:82
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
(Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa ) Surat Yaasini:82
5:Mazingatio katika Mapenzi:
Anasema Mtume-rehema na amani ziwe juu yake-
(لا يؤمن أحدكم حتى أكون أحب إليه من ولده ووالده والناس أجمعين)
(Hato amini mmoja wenu mpaka anipende kulikoni mtoto wake na mzazi wake)
Mja hawezi kuwa mkamilifu wa imani mmpaka ampende mtume kulikoni watoto zake na wazazi wake.
Mapenzi haya ndiyo yaliyo mfanya Abubakari-radhi za Allah ziwe juu yake-alie kutokana na furaha kwa kuungana na mtume katika safari hii.
Mapenzi haya ndiyo yaliyo mpelekea Abubakari avumilie maumivu ya kung`atwa na nyoka pasina ya kutikisika kwa kuwa mtume kalala juu ya miguu yake,pindi walipo kuwa pangoni.
Mapenzi haya ndiyo yaliyo pelekea Abubakari kutoa mali yake yote kwa ajili ya mtume na uislamu kulikoni kutoa katika nafsi yake na familia yake.
Mapenzi haya ndiyo yaliyo wafanya Maanswaari wakawa wakitoka nje ya Madina kila siku kipindi cha joto na jua kali wakimsubiri Mtume huenda akatokea.
Tupo wapi tunaodai kumpenda Mtume hali ya kuwa tukimuasi usiku na mchana na kujiweka mbali na suna zake???
6:Mazingatio katika kujitolea na kujitoa muhanga.
Hakika mtume na maswahaba wake wametuachia kurasa zenye kung`ara juu ya masuala ya kujitolea,sawa iwe ni kujitolea mali au hata nafsi kwa ajili ya kuinusuru dini hii tukufu.
Walihama kwa ajili ya Allah pasina ya kujitetea ya kwamba wana watoto wadogo au hawana mali za kuwatosheleza au…
Kwani dunia ilikuwa haina thamani yoyote kwao ukilinganisha na Amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake.
Tukumbuke pindi Ally radhi za Allah ziwe juu yake alipo lala katika kitanda cha mtume na kujifunika,hali ya kuwa anajua ya kwamba makafiri wa kikuraishi wapo nje na mapanga na huenda muda wowote wakaingia na kumpiga mapanga aliye lala katika kitanda kile,kwani kitanda kile kilikuwa ni cha mtume
Swalla Allahu alayhi wasallam.
Na tukumbuke pindi familia ya Abubakari walipo kuwa wakiwafanyia Mtume na Abubakari huduma mbali mbali pindi walipokuwa pangoni,bila shaka walikuwa wakijua ya kwamba iwapo kama watagundulika basi huenda wakauwawa na makafiri ,lakini hata hivyo hawakujali.
Hivi ndivyo walivyokuwa vijana wa maswahaba,tupowapi vijana wa leo na kujitolea huku na kushikamana na na kujivunia uislamu? Baadhi yetu hata kutekeleza ibada ya swala tu imekuwa ni shughuli ngumu ,je tutaweza kujitolea nafsi zetu???
Bila shaka vijana wenzangu kuna haja ya kuzinduka na kubadilisha mwelekeo, kwani tunako elekea siko!
7:Mazingatio juu ya uelevu mbinu na kuchukua sababu.
Alikuwa Mtume-rehema na amani ziwe juu yake-ni mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu,mwenye yakini juu ya nusura yake na mwenye kujua ya kwamba Allah ni mwenye kumtosheleza.
Lakini licha ya hayo yote mtume hakuwa ni mtu mwenye kupuuzia na mwenye kufanya mambo kienyeji enyeji.Bali mtume aliandaa mbinu zilizokuwa ni madhubuti kisha akazitekeleza kwa hali ya usiri na umakini wa hali ya juu.
Kiongozi wa msafara:Muhamadi
Msaidizi: Abubakari
Mtu wa kujitolea muhanga:Alliy.
Masuala ya chakula:Asmaa bint Abibakari.
Masuala ya habari:Abdallahi bin Abibakari.
Kuwapoteza maadui:Aamir.
Mtaalamu wa njia:Abdullahi bin Ariikat.
Sehemu ya kukaa kwa muda:Pango la thawri.
Muda wa kuondoka:Baada ya siku tatu.
Njia ya upitaji:Kando kando ya bahari.
Yote haya ni dalili tosha juu ya uelevu mbinu na hekima za mtume rehema na amani ziwe juu yake anazo tufundisha umma wake.Na ndani yake kuna wito kwa umma wa kiislamu juu ya kupangilia mambo yao,kuyafanya kwa umakini na kuandaa sababu za kufanikisha mambo hayo licha ya kumtegemea Allah mpitishaji wa sababu zote mwanzo mpaka mwisho.
8:Mazingatio juu ya Ikhlasi.
Alikuwa Abubakari radhi za Allah ziwe juu yake akitoa mali zake kwa mtume na katika ulinganiajia wa dini ya Allah na katika majukumu mbali mbali ya uislamu.
قال الله تعالي(الذي يؤتي ماله يتزكى )سورة الليل:18
Anasema Allah Mtukufu kwa kumsifu Abubakari:
(Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa)
Surat Allayli:18
Na katika safari hii Abubakari aliandaa vipandwa kwa gharama zake lakini mtume akamkatalia na kumrudishia thamani yake.
9:Mazingatio juu ya tarehe ya kiislamu:
Waisalamu kuwa na terehe yao ni jambo miongoni mwa mambo yenye kupelekea utukufu wa waislamu na kutofautiana mila nyingine.
Asili ya kuanzishwa kwa tarehe ya kiislamu ni kipindi cha khalifa wa mtume Omari bin Khatwabi radhi za Allah ziwe juu yake.
Omari alipata fikra hii ya waislamu kuwa na tarehe yao itakayo kuwa ikitofautiana na watu wengine.Akawataka ushauri maswahaba,wakajadili juu ya suala hili ,je tarehe hii ianzie wapi?
Je tokea kuzaliwa kwa mtume? Au baada ya kupewa utume?au baada ya kuhama? Au baada ya kufariki?
Wakaafikiana ya kwamba tarehe ya kuhama ndilo chaguo munasibu.
Kwani kuzaliwa kwake mtume na muda wa kutumwa kwake ni masuala ambayo wanazuoni wametofautiana.
Ama muda wa kufariki kwake bila shake suala hili litapelekea huzuni kwa waislamu,kwani hakuna msiba mkubwa zaidi ya kufiwa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Kwahiyo Allah akawaongoza maswahaba juu ya kuchagua tarehe hii ya kuhama kwa mtume.
Na waislamu wakashikamana nayo karne baada ya karne mpaka kufika muda huu ambao waislamu tumesahau kabisa tarehe yetu na wala hatuitilii umuhimu.Tumekuwa hatuikumbuki tarehe hii isipokuwa mwezi wa ramadhani au miezi ya hijja.

0 comments:
Post a Comment